Posts

Showing posts from February 8, 2018

listen & Download New Audio | Kcee ft. Sarkodie – Burn

Image

New AUDIO: Orezi ft. Tekno – Whine For Daddy

Image
Orezi collaborates with Tekno on his first single of 2018 titled ‘Whine for Daddy.’ The song comes after his 2017 hit songs, ‘Hallelujah’ and ‘ Cooking Pot ’. Orezi describes ‘Whine for Daddy’ as a “Sugar Daddy jam” aimed at making people dance. According to him, “I was just trying to make a record that people can dance to, just whine and Daddy will take care of you.”

“Mimi ni msichana nataka kubembelezwa” - Chemical

Image
Msanii wa kike wa hip hop bongo Chemical, kwa mara ya kwanza amezungumzia maisha yake ya kimapenzi, kitu ambacho ni nadra sana kwa msanii huyo kufanya hivyo.   Akizungumza na team ya Planet Bongo ya East Africa Radio,  Chemical amesema yeye kama msichana ana hisia za mapenzi na anajua kupenda, ila anahofia kuumizwa hivyo hawezi nguvu nyingi kwenye masuala ya mapenzi. “Unajua kuna mambo mengine tunayafanya kwenye muziki kuweza kuweka image nyingine, ila mi niko tofauti na niko real, ukisikiliza nyimbo zangu nyingi Chemical anajua kupenda, anataka kubembelezwa, mi msichana jamani, na mapenzi yapo, ila mimi nahisi nina vitu vini vya kufocus kiasi kwamba kwenye mapenzi sitii nguvu nyingi, sipendi moyo wangu uumie”, amesema Chemicla. Chemical amefunguka hayo baada ya tetesi kuwa mpenzi wake alikuwa akiishi naye pamoja ambaye pia anayemsimamia, kutokea kutoelewana kiasi cha kususa kumsimamia kazi zake bila taarifa yoyote, licha ya kwamba ...

"Nisijekufa nipo CCM nikaishia motoni"-Tambwe Hiza

Image
Mhe. Freeman Mbowe amefunguka na kusema kuwa amesikitishwa na taarifa ya kifo cha Tambwe Richard Hizza na kudai kuwa alipotoka CCM na kwenda upinzani kwake yeye ni kama alikuwa anatubu kwani hakutaka kufa akiwa ndani ya CCM.  Mbowe amesema hayo leo Februari 8, 2018 baada ya kusikia taarifa ya kifo cha Tambwe Richard Hizza ambaye amefariki ghafla usiku wa kuamkia leo  "Nimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Kamanda Tambwe Richard Hizza, Kamanda mwingine tena amelala.Kamanda vita vizuri umepigana, safari umemaliza, hakika umesimama imara kuipigania demokrasia, hakika Taifa litakukumbuka kwa uthubutu wako wa kuikemea Serikali katika mabaya bila woga ingawa tulikuwa kwenye kipindi ambacho kumekuwa na kuminywa kwa haki ya kutoa mawazo na kuikosoa Serikali bila hofu"  Kufuatia kifo cha Hizza Mwenyekiti wa CHADEMA amedai wao ili kumuenzi kamwe hawawezi kurudi nyuma bali watasimamia yale wanayoyaamini ili kumuenzi na kufikia matamanio ambayo kiongozi h...

Mtulia amkana Salum Mwalimu hadharani

Image
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia amemkana mgombea ubunge wa CHADEMA, Salum Mwalimu kwamba hakuwahi kumpigania kwa namna yoyote wakati wa uchaguzi mkuu 2015 alipokuwa mgombea wa jimbo hilo kupitia CUF chini ya mwamvuli wa UKAWA.   Leo asubuhi kupitia kipindi cha East Africa Breakfast ndani ya EA radio Mtulia ambaye ni mgombea wa Ubunge wa Knondoni kupitia CCM  ameyasema hayo wakati akijibu swali la Salum Mwalimu ambaye ni mshindani wake kwa sasa katika uchaguzi huo kupitia CHADEMA, baada ya kumuuliza anajisikia vipi baada ya kuwasaliti wana kinondoni ambao,  baadhi yao walipoteza maisha yao  wengine kubaki vilema na hata wajawazito kupoteza mimba zao wakati wakishinikiza mgombea wao (Mtulia) atangaziwe ushindi 2015. Mtulia amesema kwamba, Mwalimu kumuambia kwamba alimpigania si kweli  kwani wakati wakati wa uchaguzi 2015, Mwalimu alikuwa anampigania mgombea mwingine wa jimbo la kikwajuni hivyo ana uhakika kwamb...

Tundu Lissu amjibu Lemutuz

Image
Tundu Lissu ametumia ukurasa wake wa Instagram kumjibu Lemutuz na kudai kuwa hajawahi kuwasiliana naye kwa namna yoyote ile na kama kweli angekuwa ni rafiki yake toka aliposhambuliwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana basi angeweza kumkumbuka japo hata kwa kumpa pole lakini hakufanya hivyo. "Leo nimeonyeshwa post iliyopo kwenye Instagram account ya William Malecela aka Lemutuz. Kwenye post yake, Lemutuz amedai kwamba mimi ni rafiki yake mkubwa na wa miaka mingi, kabla vijana wengi wanaopiga makelele mitandaoni hawajazaliwa. Lemutuz ameeleza kwamba mwaka 2010 alinipokea Uwanja wa Ndege wa John F. Kennedy, mjini New York, nilipoenda kwenye mahafali ya dada yangu. Naomba kuweka ukweli wa kauli za Lemutuz wazi ili kuweka rekodi sawa. Kwanza, nimemfahamu Lemutuz tangu mwezi Mei, 2011. Nilikutana naye mara ya kwanza kwenye mahafali ya mdogo wangu kaka (sio dada) Vincent Mughwai, aliyekuwa anasoma Bridgeport University (sio Connecticut State University). Kama nakum...

Mange Kimambi ahesabiwa siku na Sheikh

Image
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Al Haji Mussa Salimu amemjibu mwanadada mkosoaji wa mtandaoni Mange Kimambi kwa kudai kuwa huu ndiyo mwaka wake wa mwisho kutumia mikono pamoja na ulimi wake kutukana watu. Sheikh huyo amesema kwamba kutokana na kitendo hicho cha Mwanadada huyo kumuanika mtandaoni na kumtolea maneno machafu yeye kama kiongozi wa dini atarudi kwenda kushtaki katika mahakama ya mbinguni ambayo haina rushwa. Kauli hiyo ya Sheikh Mkuu imekuja ikiwa ni siku moja tangu ianze kusambaa picha yake mitandaoni na kuanza kutuhumiwa kuwa anashiriki katika kampeni za uchaguzi mdogo kukisaidia Chama Cha Mapinduzi " Tutarejea katika mahakama ya mbinguni kwani mahakama ya Mwenyezi Mungu haina rushwa na tutamuuliza  Mwenyezi Mungu kama alimpa Huyu Mange Kimambi ulimpa mikono kwa ajilli ya kudhalilisha na kuvunja heshma za watu. Amekuwa akiwatukana viongozi wa serikali lakini kwa hekima zao wamemnyamazia kimya"  Al Haji Mussa Salimu . Ameongeza kwamba " Tun...

Mfahamu Mfalme Mswati na wake zake

Image
Mfalme wa Swaziland Makhosetive Dlamini maarufu kama King Mswati, wakati anateuliwa kuwa mfalme kurithi kiti cha Baba yake Mfalme Sobhuza III. King Mswati alikuwa ndiye mtu mdogo zaidi kuongoza nchi za kifalme duniani, kwani alikuwa na miaka 18 tu. Mpaka sasa ana jumla ya wake 14 na watoto 24, wake zake wawili huchaguliwa na wazee wa nchi ambao hujulikana kama bodi, na lazima wawe wametoka kwenye familia zenye status nzuri. Mke wake wa kwanza 'Queen LaMatsebula'  ndiye anayehusika na masuala yote ya kiserikali, na lazima atokee kwenye familia yenye uwezo au wa kichifu, na awe na tabia na siha njema. Lakini licha ya kuwa ndiye mke mkubwa, mtoto wake wa kiume haruhusiwi kurithi kiti cha baba yake. Kitaaluma huyu ni mwanasaikolojia. Mke wake wa pili Queen LaMotsa “La Madone”  ambaye ni Patron wa shule ya wasichana ya Mt. Annes ya Malkerns na pia ni balozi wa UNDP, huyu huchaguliwa na bodi ya taifa (unaweza sema baraza la wazee) kuwa mke wa M...

Korea kaskazini imezindua pombe mpya ya kipekee

Image
Kwa mujibu wa gazeti la serikali   Rodong Sinmun , kiwanda cha kutengeneza pombe nchini Taedonggang kinadai kuwa mbinu yake mpya ya kutumia ngano badala ya mpunga ni bora zaidi kuliko pombe nyingine zilizoko kwa ladha na hata harufu nakwamba imepokewa vizuri na waraibu nchini. Taedonggang kimekuwa kikitengeneza pombe tangu mwaka 2015, na hii huenda inatokana na shutuma kutoka kwa kiongozi mkuu nchini Kim Jong-un kwamba pombe inayoingizwa nchini kutoka Korea kusini haina ladha, jarida la kila siku huko Seoul Chosun Ilbo liliripoti wakati huo. Haki miliki ya picha KIM WON-JIN/AFP Kwa kawaida, vyombo vya habari Korea kaskazini vinaitangaza pombe hiyo kama ufanisi katika mpango wa Kim Jong-un kuinusha viwango vya maisha katika nchi hiyo ya kikomyunisti, vikisema ni kutokana na ' jitihada za muda wote"kuyafanya maisha "kuwa ya raha zaidi kwa raia".

Mwanamuziki Rihanna hatakiwi kufika ghana

Image
Mwanamuziki wa kimataifa Rihanna anategemewa kuhudhuria mkutano mkubwa nchini Senegal,lakini vikundi vya dini nchini humo wamekataa kumpokea, chombo ch habari cha Jeune Afrique kimeripoti. "Tumeukataa ufreemason na mapenzi ya jinsia moja" , shirika la vikundi 30 vya kidini wamesema, wakimshutumu mwaimbaji huyo kwa kutumia ishara za mazo na kuwa mjumbe wa chimbuko la Illuminati , lilanoaminika kuwa ni kundi maalum la watu ambao hudhibit masuala na uongozi wa dunia na inasadikika kuwa hufanya shughuli zao kisiri kudhibiti kila kitu na kuunda Utawala Mpya wa Dunia. Shutuma hizo zimefutiliwa mbali na wasanii waliowahi kufanya nao kazi huko nyuma, Rihanna atatembelea nchi hiyo ya Afrika Magharibi akiwa katika nyadhifa yake ya balozi wa shirika la elimu 'Global Partnership Foundation' Shirika hilo linamaadhui wa kuchangisha fedha za kuwafundishia mamilioni ya watoto na vijana katika nchi zinazoendelea. Chombo cha habari cha Jeune Afrique kimemnukuu Waziri wa M...

Korea Kaskazini kuonyesha uwezo wake wa kijeshi kabla ya Olimpiki

Image
Taifa la Korea Kaskazini linatarajiwa kuandaa maadhimisho ya 70 ya gwaride la jeshi lake kabla ya kufanyika kwa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi nchini Korea Kusini. Gwaride la kila mwaka la Pyongyang linaloadhimisha kuanzishwa kwa jeshi la Korea Kaskazini limekuwa likifanywa kila mwezi Aprili kwa kipindi cha miaka 40. Hatahivyo vyombo vya habari nchini humo vilitangaza mapema mwaka huu kwamba tarehe ya kufanyika kwa gwaride hilo la kijeshi imebadilishwa hadi Februari 8. Korea Kaskazini imepuuzilia mbali ukosoaji wa mpango wake ikisema kuwa hakuna mtu aliye na uwezo wa kuishutumu. ''Ni utamaduni na swala muhimu sana kwamba kila taifa duniani linasherehekea uzinduzi wa jeshi lake' , kilisema chama tawala cha wafanyikazi Rodong Sinmun.

TANZIA: Mwanasiasa maarufu, Richard Tambwe Hizza afariki Dunia

Image
Mwanachama wa CHADEMA, Richard Tambwe hiza amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake. Mwili wake umepelekwa Hospitali ya Temeke Dar Es Salaam asubuhi hii. Hadi jana saa tano usiku alikuwa kwenye Kikao cha CHADEMA. Marehemu Tambwe Hizza amefariki akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa pumu na amefariki akiwa ni mmoja wa waratibu wa kampeni za chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) katika jimbo la Kinindoni Hizza anafahamika sana kwa siasa zake akiwa CUF, Baadae alihamia CCM na kuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda wa CCM na 2015 aliamua kuondoka CCM na kuhamia CHADEMA. Mwaka 2014 alisema angegombania Urais kupitia cha mapinduzi kwani ana uwezo, akili, elimu na  afya ya kumuwezesha kuwa Rais wa tano wa Tanzania. Jana alishiriki kampeni za kumnadi Salum Mwalimu Tandale mapema jioni kabla ya Vikao vya chama..

Mwanaume aiba figo ya mkewe, akitaka alipwe mahari

Image
 Mume wa mwanamke mmoja nchini  India  pamoja na kaka yake wamekamatwa na polisi baada ya mke wa mwanaume huyo kuwashtaki kuwa wamemuibia figo yake bila kujua ikiwa kama gharama ya mahari ya ndoa yao hiyo. Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa miaka miwili iliyopita mwanamke huyo alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya kidole tumbo (appendicitis) na ikabidi afanyiwe upasuaji na mchakato mzima wa matibabu hayo ya upasuaji ulifanywa na mwanaume huyo. Mwaka 2017 mwishoni mwanamke huyo alipofanyiwa uchunguzi na Madaktari iligundulika kuwa hakuwa na Figo yake moja jambo ambalo mwanamke huyo  Rita Sarkar  ameliunganisha na mgogoro wa kutolipa mahari kwa mumewe. Nchini India kiutamaduni mwanamke akitaka kuolewa, huwa analipa mahari kwa familia ya mwanaume anayetaka kuolewa naye. Japokuwa sheria hii ilishafutwa tangu mwaka 1961 mwanamke huyo amedai kuwa amekuwa akifanyiwa unyanyasaji na mumewe kutokana na kutolipa mahari hiyo walipokuwa wakioana.

“Prof Ndalichako si ungekuwa Waziri wa masifuri?” –Mbunge Goodluck Mlinga

Image
Goodluck Mlinga ambaye ni Mbunge wa Ulanga ni miongoni mwa Wabunge ambao siku zote wakisimama kuchangia Bungeni hawakosi kuacha headline, sasa leo alisimama kuchangia mapendekezo ya taarifa mbili zilizowasilishwa Bungeni ikiwemo taarifa ya kamati ya kudumu ya maendeleo ya jamii pamoja na taarifa ya kudumu ya Bunge kuhusu masuala ya UKIMWI. Sasa leo kashauri Bora Rais Magufuli ateue Waziri wa elimu ambaye hajasoma kabisa.