Mwanaume aiba figo ya mkewe, akitaka alipwe mahari

 Mume wa mwanamke mmoja nchini India pamoja na kaka yake wamekamatwa na polisi baada ya mke wa mwanaume huyo kuwashtaki kuwa wamemuibia figo yake bila kujua ikiwa kama gharama ya mahari ya ndoa yao hiyo.
Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa miaka miwili iliyopita mwanamke huyo alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya kidole tumbo (appendicitis) na ikabidi afanyiwe upasuaji na mchakato mzima wa matibabu hayo ya upasuaji ulifanywa na mwanaume huyo.
Mwaka 2017 mwishoni mwanamke huyo alipofanyiwa uchunguzi na Madaktari iligundulika kuwa hakuwa na Figo yake moja jambo ambalo mwanamke huyo Rita Sarkar ameliunganisha na mgogoro wa kutolipa mahari kwa mumewe.
Nchini India kiutamaduni mwanamke akitaka kuolewa, huwa analipa mahari kwa familia ya mwanaume anayetaka kuolewa naye. Japokuwa sheria hii ilishafutwa tangu mwaka 1961 mwanamke huyo amedai kuwa amekuwa akifanyiwa unyanyasaji na mumewe kutokana na kutolipa mahari hiyo walipokuwa wakioana.

Comments

Popular posts from this blog

DOWNLOAD NA USIKILIZE NYIMBO ZA KWARESIMA