Dar es Salaam. Wakati madiwani wa Chadema wakiendelea kuhamia CCM, viongozi wakuu wawili wa chama hicho wametoa sababu za wanasiasa hao kufanya hivyo. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema madiwani hao wanahama kwa sababu walitarajia kupata masilahi binafsi ambayo wameyakosa. “Waliojiunga na Chadema kufuata masilahi wamekuta hakuna, hapa ni wito, ndiyo hao wameondoka,” alisema. Wakati Mbowe akisema hayo, katibu mkuu wake, Vincent Mashinji amedai makada hao wanahama kwa ahadi ya kulipiwa mikopo wanayodaiwa kwenye taasisi za fedha. “Baadhi ya madiwani walikuwa wanadaiwa mikopo na taasisi za fedha, sasa wamelipiwa baada ya kununuliwa,” alisema. Kauli za viongozi hao zimekuja siku moja baada ya diwani wa Chadema, Kata ya Kaloleni mkoa ni Arusha, Emmanuel Kessy kujiuzulu juzi saa sita usiku na kujiunga na CCM huku akitoa sababu tatu za uamuzi huo. Kessy ambaye anakuwa diwani wa 22 kuhama chama hicho mkoani Arusha alitaja sababu hizo kuwa ni kumuunga mkono Rais Jo...