Posts

Showing posts from February 14, 2018

MKRISTO USIOGOPE KIFO JIANDAE KWA KIFO CHEMA

Image
Makala hii ni sehemu ya Kitabu cha Kalamu kwa Vijana ambacho kipo katika hatua za mwisho kuchapishwa. Mwandishi ameamua kutoa sehemu hii ya makala isomwe na watu wote baada ya tukio la ajali ya kusikitisha iliyopoteza maisha ya watoto 29. Haki zote za mwandishi zimehifadhiwa . Utangulizi Kati ya mambo ambayo binadamu tunayaogopa sana mojawapo ni kifo, mwanadamu anaogopa kifo kwa kuwa kwanza kinamtenga na familia yake, ndugu, jamaa marafiki ambao amezoeana nao, pili anaogopa kifo kwa kuwa hafahamu ni wapi anapoelekea, jambo lingine linalowaogopesha watu juu ya kifo ni kuyaacha mambo ya dunia na raha zake ambazo amekua akizihangaikia kwa muda mrefu sana, kifo huogopwa pia kutokana na hukumu kwa wale wanaoamini uwepo wa Mungu na hukumu yake. Mwanadamu anapofariki huku nyuma huacha majonzi na simanzi kubwa haswa kwa wale waliokua wanamtegemea na wote ambao kwa namna moja au nyengine walikua wanafaidika na uwepo wake hapa duniani. Kifo cha kijana mara nyingi huwa ni pigo zaidi, m...

IJUE KWARESMA NA MISINGI YAKE

Image
*TUMSIFU YESU KRISTO? * Leo nakukaribisha ujifunze kuhusu kipindii tunachoelekea* " Ijuwe jumatano ya majivu kiundani " Jumatano ya Majivu, katika kalenda ya mwaka wa Kanisa la Magharibi, ni siku ya kwanza ya kwaresima, walau kwa madhehebu mengi. Jina linatokana na desturi ya kumpaka mtu majivu kichwani pamoja na kumtamkia maneno ya kumhimiza afanye toba inavyotakiwa na kipindi hicho cha liturujia kinachoandaa Pasaka. Kwa kawaida siku hiyo unaanza mfungo unaofuata kielelezo cha Yesu kufunga chakula siku arubaini jangwani baada ya kubatizwa na Yohane Mbatizaji na kabla ya kuanza utume wake mwenyewe. Wakati umetimia na ufalme wa Mungu umekaribia, tubuni na kuiamini Injili, (Mk 1:15), haya ndiyo maneno ya kwanza ya Yesu ambayo kadri ya Mwinjili Marko yanafungua kazi ya hadhara ya Yesu, kwa maana hiyo kazi ya Yesu inaanza kwa kuwaandaa watu katika toba ili hatimaye, wapate kuukaribia au kuingia katika ufalme wa Mungu. Na wakati ndiyo sasa. Wakati ni sasa , Yesu anatuhubiria n...

DOWNLOAD NA USIKILIZE NYIMBO ZA KWARESIMA

Image
NYIMBO ZA KWARESIMA Zifuatazo ni nyimbo mbalimbali za kwaresima, unaweza kusikiliza na kudownload, bonyeza wimbo unaoutaka na moja kwa moja ukurasa mpya utafunguka utakao kuwezesha kusikiliza nyimbo hiyo, na juu kabisa kutakua na alama inayokuonesha kudownload bonyeza alama hii ipo juu kabisa. . Ukipata tatizo jaribu kubadilisha browser unayotumia kudownload. Karibu ASIREGEE MOYOWE BWANA KAMA WEWE UNGEHESABU MAOVU YETU BWANA NI KINGA NA NGAO YANGU EE BWANA USIKIE KABILA LANGU KRISTO ALIJINYENYEKEZA KRITO AMEKUA MTII  KWA ISHARA YA MSALABA KWA NINI WASIMAMA MBALI LAUMU IMEUVUNJA MATESO YAKO MSALABANI MTAZAME MWOKOZI MUNGU WANGU MUNGU WANGU MBONA UMENIACHA NIMEKUKIMBILIA PASIPO MAKOSA TUKOMBOE TUMEKOSA KWELI WAKUPELEKA HUKUMUNI YESU WANGU YESU AKALIA KWA SAUTI KUU