Posts

Showing posts from February 16, 2018

"Tumemchukulia hatua tayari" - Muliro

Image
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Muliro J. Muliro amefunguka na kusema kuwa wamemchukulia hatua za kinidhamu askari polisi wake mmoja ambaye jina lake halijawekwa wazi kufuatia kuonekana akichukua rushwa kwenye video za mitandaoni. Hatua hiyo ya jeshi la polisi imekuja masaa kadhaa baada ya Mwanaharakati wa mambo ya siasa mtandaoni, mrembo Mange Kimambi kuposti video ya askari polisi akichukua rushwa ya pesa kutoka kwa raia ambaye alitenda kosa la barabarani. Akithibitisha juu ya kuchukua za kinidhamu kwa askari huyo Kamanda Muliro amesema ni kweli Jeshi la Polisi limechukua maamuzi hayo kwa askari huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake.  "Ni kweli tumechukua hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria na kanuni za kipolisi kwa askari yule, kuhusu jina lake kwa sasa hatuwezi kuliweka wazi kwa kuwa jeshi la polisi haliwezi kufanya kazi kwa matangazo"  alisema Muliro 

Polepole atoa siri ya ushindi wa uchaguzi wa kesho

Image
Humphrey Polepole Polepole ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mdogo wa marudio wa Ubunge na nafasi za udiwani ambao unatarajia kufanyika (kesho) Februari 17. 2018 na kudai sababu kubwa za upinzani kushindwa ni kutokana na wao kuwa wabinafsi. "Napenda ifahamike kwa herufi kubwa, ni kawaida ya CCM kushinda na tunashinda kwa sababu tumefanya kazi nzuri ya kushughulika na shida za watu na watu wameona, wanatupenda, wanatuheshimu, wanatuthamini na wakati wote wanatupa kura nyingi za kishindo",  amesema Polepole. Pamoja na hayo, Polepole ameendelea kwa kusema  "nitoe rai kwa vyama vya upinzani kuwa na uvumilivu kwa sababu ni kawaida yao kushindwa, kutokana na wao hawashughuliki na shida za watu, wamekuwa wabinafsi wanajitizama wao wenyewe, wamekuwa wapinga maendeleo kwa kila jambo jema linalofanywa. Rai yangu unaposhindwa kuwa na uvumilivu". Kwa upande mwingine, Polepole amesema vyama vya upinzani ...

"Hatua zinachukuliwa kwa wapinzani tu" – Mlinga

Image
Mbunge wa jimbo la Ulanga kupitia CCM Goodluck Mlinga, amesema kwamba tabia ya kuchukuliana hatua pale mbunge anapomsema vibaya kiongozi mkubwa, haiko kwa wabunge wa CCM isipokuwa kwa upinzani ndiyo hawawezi sema ukweli watachukuliwa hatua na viongoz Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, Mlinga amesema wao kama chama wanakosoana na hakuna anayechukuliwa hatua, isipokuwa vyama vya upinzani ndio wana tabia ya kuchukuliana hatua pale mbunge anapoongoea ukweli kuhusu chama, akimtolea mfano Zitto Kabwe wakati akiwa CHADEMA. “CCM hakuna hiko kitu kwamba ukisema utaitwa kwenye kikao, hivyo vitu nenda vyama kama CHADEMA au ACT huko, CCM hamna hiko kitu, nishawahi kurusha mawe, nishawahi kusema Mheshimiwa Rais uliposhika ni pabaya, sikuwahi kupigiwa hata simu na tukikutana tunagonga tano kama kawaida, CCM hakuna hiko kitu, chama chetu sisi tunapelekeana moto kama kawaida”, amesema Mlinga. Mbunge huyo ambaye...

Waziri amjibu Mange Kimambi

Image
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amefunguka na kujibu hoja ambayo Mwanaharakati wa mambo ya siasa mtandaoni, Mange aliibua kwenye mtandao wake Instagram kudai Waziri huyo ameshiriki kuwaingiza chaka Watanzania ili watapeliwe pesa Waziri Kigwangalla akijibu hoja hiyo amesema kwamba yeye alialikwa kama mgeni wa heshima na kuwa alikuwa hawatambui watu hao binafsi na wala biashara yao alikuwa haitambui na alipoitwa kuzindua tawi lao hapa nchini alishindwa kuwakatalia ila hana maslahi binafsi katika kampuni hiyo.   "Nimeona nitoe ufafanuzi kwenye hili jambo. Maana kila mjadala juu ya hii kampuni ya ..... unapoibuka, jina langu linakuja, na mara nyingine picha yangu inawekwa. Ukweli ni kwamba, nilialikwa kwenye shughuli ya uzinduzi wake kama mgeni wa heshima; mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa wakati huo, Dr. Adelhelm Meru. Niliamini kwa heshima ya kuzinduliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viw...

Hashim Rungwe aungana na CHADEMA

Image
Mheshimiwa Hashim Rungwe Spunda Mwenyekiti  (CHAUMMA) jana Februari 15, 2018 aliungana na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kumnadi mgombe Ubunge wa CHADEMA katika jimbo la Kinondoni  Salum Mwalimu. Akiwa kwenye mkutano huo ambao ulifanyika katika Kata Ya makumbusho Viwanja Vya Vegas Rungwe alisema kuwa wana Kinondoni hawapaswi kumchagua mgombea wa CCM kwa kuwa ni msaliti na amekuwa muongo.  "Serikali hii ya CCM inajidai sanaa inafanya propaganda kwenye Radio na kila mahali lakini mimi naomba niulize wangapi wamekuja hapa hawana kitu mfukoni, mna hela nyie? Wananchi hali zao mbaya watu hawana kitu. Jamani tunampima kiongozi kwa mambo anayofanya tumeona tawala nyingi lakini mmeshawahi kuona utawala wa namna hii? Yaani polisi ndiyo wanafanya serikali ifanye kazi yaani bila ya polisi hawafanyi kazi, polisi ndiyo wamewekwa mbele yaani ukisema hivi unakamatwa"  Rungwe aliendelea kuelezea juu ya sakata lake la kukamatwa na p...

Cyril Ramaphosa aapishwa kuwa rais wa Afrika Kusini

Image
Sambaza habari hii Me Sambaza h Haki miliki ya picha Mwenyekiti wa chama tawala cha ANC Cyril Ramaphosa amepishwa kuwa rais wa Afrika Kusini baada ya rais wa taifa hilo Jacob Zuma kujiuzulu. Rais huyo mpya alikuwa mtu wa pekee aliyeteuliwa siku ya Alhamisi huku uteuzi huo ukiungwa mkono kwa shangwe bungeni. Bwana Zuma alikuwa chini ya shinikizo kali kutoka kwa chama chake cha ANC kilichomtaka ajiuzulu la sivyo akabiliwe na kura ya kutokuwa na imani dhidi yake bungeni. Katika taarifa ya runinga, alisema kuwa anajiuzulu mara moja lakini hakubaliani na uamuzi wa chama. Bwana Zuma anakabiliwa na madai kadhaa ya ufisadi lakini amekana kufanya makosa yoyote. Akiwa naibu wa rais Ramaphosa anakuwa kaimu wa rais mara moja baada ya Zuma kujiuzulu. Taarifa ya serikali inasema kuwa bunge litamchagua rais mpya wa Afrika Kusini Alhamisi jioni. Bwana Zuma ,mwanachama wa jeshi la ANC wakati wa ubaguzi wa rangi, alipitia nyadhfa kadhaa za chama hicho hadi kuwa rais. Aliliongo...

Mtoto azaliwa na risasi mwilini nchini Marekani

Image
Mtoto mmoja amezaliwa na risasi ndani ya mwili wake katika jimbo la Tenesee nchini Marekani. Mamake mwenye umri wa miaka 19 alipigwa risasi katika kisa kimoja kilichohusisha magari mawili barabarani karibu na mji wa Memphis , kulingana na vyombo vya habari. Mwanamke huyo alikuwa na ujauzito wa wiki 36 wakati alipopigwa risasi. Alipelekewa hospitalini ambapo alihitaji kufanyiwa upasuaji na ndiposa akajifungua mwanawe. Mtoto huyo alizaliwa na majeraha akiwa katika hali mahututi, kulingana na maafisa wa polisi wa Memphis. Mwanamume aliyeandamana na mwanamke huyo hospitalini aliambia maafisa wa polisi kwamba watu watatu waliokuwa katika gari jeusi aina ya Chevrolet walikaribia gari lao barabarani kabla ya kuwafyatulia risasi kulingana na chombo cha habari cha Fox 2 News. Mama huyo alipigwa risasi mara tatu katika nyonga yake ya kulia, kituo hicho kiliripoti

Lupita: sikuwahi kusikia hata filamu moja ya ushujaa yenye watu weusi

Image
Nyota wa filamu Black Panther, Lupita Nyong'o katika uzinduzi wa filamu hio Ulaya Filamu ya Black Panther bado inaendelea kuwa gumzo. Leo hii imezinduliwa jijini Johannesburg Afrika Kusini na sehemu menignio barani Afrika . Filamu hii inahusu mji wa kufikirika wa Kiafrika na imesheheni waigizaji wenye asili ya Afrika. Mwandishi wa BBC Kim Chakanetsa amezungumza na mmoja wa nyota wa filamu hiyo Lupita Nyong'o. Alianza kwa kumuuliza kwanini ni muhimu kwake kushiriki katika filamu hii? Lupita:  Tangu mwanzo kabisa wakati Ryan aliponiambia juu ya maudhui ya filamu hii, sikuamini - sikuwahi kuskia hata filamu moja ya ushujaa ya namna hii. Nikamuuliza "Una uhakika Marvel wamekubaliana na simulizi hii? Akasema ndio ndio, wamekubali. Kikubwa katika filamu hii ni kwamba haijaogopa kugusia masuala ya msingi na ya kina ya kijamii na kisiasa na kwa kweli inaendana kabisa na ulimwengu wetu huu wa leo Kim:  Huko nyuma palikuwa na malalamiko jinsi gani ambavyo Afrika inaony...

Saa 48 zilizomng'oa Zuma

Image
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amejiuzulu baada ya shinikizo nyingi kutoka kwa chama chake. Hatimaye Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ajiuzulu Kapitia hotuba yake iliyopeperushwa kwa njia ya televisheni alisema anajiuzulu mara moja lakini akaongeza kuwa hakubaliani na uamuzi wa chama cha ANC. Chama cha ANC kilikuwa kimemuambia aondoke madarakani au akabiliwe na kura ya kutokuwa na imani naye bungeni. Jacob Zuma: Sijafanya makosa ya mimi kujiuzulu Wasifu wa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma Zuma mwenye umri wa miaka 75 amekuwa akikabiliwa na shinikizo za kumtakja ampe nafasi mamamu wake Cyril Ramaphosa, ambaye ndiye sasa kiongozi mpya wa chama. Bw Zuma ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2009, amekumbwa na shutuma nyingi za ufisadi. Mapema Jumatano, polisi walivamia nyumba ya familia tajiri ya Gupta ambayo Zuma ana uhusiano wa karibu nayo. Zuma alijiuzulu kwa njia gani? Alianza hotuba kwa kucheka na kufanya mzaha na waandishi wa hahari. Baada ya kuwashukuru ...

Florida shooting: Nikolas Cruz confesses to police

Image
The teenager accused of killing 17 people at a Florida high school on Wednesday has confessed to the shooting, police say. Nikolas Cruz, 19, said he arrived on campus and began shooting students before abandoning his weapon and escaping, according to a court document. He has appeared in court charged with 17 counts of premeditated murder. The FBI has admitted it received a tip-off about him last year. The attack, at Marjory Stoneman Douglas High School in Parkland, Florida, is the deadliest US school shooting since 2012. Who are the victims? How the school attack happened Analysis: One shooting, two Americas " Cruz stated that he was the gunman  who entered the school campus armed with a AR-15 and began shooting students that he saw in the hallways and on the school grounds," according to the court document. He said he was carrying extra ammunition in a black duffel bag and backpack, it said. Mr Cruz then discarded his weapon in an attempt to blend i...