Polepole atoa siri ya ushindi wa uchaguzi wa kesho
Polepole ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mdogo wa marudio wa Ubunge na nafasi za udiwani ambao unatarajia kufanyika (kesho) Februari 17. 2018 na kudai sababu kubwa za upinzani kushindwa ni kutokana na wao kuwa wabinafsi.
"Napenda ifahamike kwa herufi kubwa, ni kawaida ya CCM kushinda na tunashinda kwa sababu tumefanya kazi nzuri ya kushughulika na shida za watu na watu wameona, wanatupenda, wanatuheshimu, wanatuthamini na wakati wote wanatupa kura nyingi za kishindo", amesema Polepole.
Pamoja na hayo, Polepole ameendelea kwa kusema "nitoe rai kwa vyama vya upinzani kuwa na uvumilivu kwa sababu ni kawaida yao kushindwa, kutokana na wao hawashughuliki na shida za watu, wamekuwa wabinafsi wanajitizama wao wenyewe, wamekuwa wapinga maendeleo kwa kila jambo jema linalofanywa. Rai yangu unaposhindwa kuwa na uvumilivu".
Kwa upande mwingine, Polepole amesema vyama vya upinzani ni kawaida yao mara zote kupinga ustawi wa watanzania pamoja na kuwa wapingaji wa maendeleo jambo ambalo ndio linawafanya kutoaminika kwa jamii kuwapa kura za ushindi.
Comments
Post a Comment