Posts

Showing posts with the label michezo

Alexis Sanchez ahukumiwa kifungo cha miezi 16 jela

Image
Mchezaji mpya wa klabu ya Manchester United Alexis Sanchez amehukumiwa jela miezi 16 kutokana na kosa la kukwepa kulipa kodi. Hukumu hiyo imetolewa jana ,Sanchez anadaiwa kukwepa kulipa kodi wakati alipokuwa nchini Uhispania ambapo mamlaka nchini humo zinasema anadaiwa kiasi cha pauni laki tisa. Kwa mujibu wa sheria za Hispania, hukumu ya kosa hilo haizidi miaka miwili jela, lakini badala yake kulipa pauni 525,000 kutokana na kosa ambalo alilifanya miaka mitatu alipokuwa akichezea klabu ya Barcelona. Hukumu ya Sanchez imekuja katika kipindi ambacho bado mamlaka za mapato nchini Hispania zinafanya uchunguzi kuhusu kocha Jose Mourinho anaye tajwa 

“Mimi ni msichana nataka kubembelezwa” - Chemical

Image
Msanii wa kike wa hip hop bongo Chemical, kwa mara ya kwanza amezungumzia maisha yake ya kimapenzi, kitu ambacho ni nadra sana kwa msanii huyo kufanya hivyo.   Akizungumza na team ya Planet Bongo ya East Africa Radio,  Chemical amesema yeye kama msichana ana hisia za mapenzi na anajua kupenda, ila anahofia kuumizwa hivyo hawezi nguvu nyingi kwenye masuala ya mapenzi. “Unajua kuna mambo mengine tunayafanya kwenye muziki kuweza kuweka image nyingine, ila mi niko tofauti na niko real, ukisikiliza nyimbo zangu nyingi Chemical anajua kupenda, anataka kubembelezwa, mi msichana jamani, na mapenzi yapo, ila mimi nahisi nina vitu vini vya kufocus kiasi kwamba kwenye mapenzi sitii nguvu nyingi, sipendi moyo wangu uumie”, amesema Chemicla. Chemical amefunguka hayo baada ya tetesi kuwa mpenzi wake alikuwa akiishi naye pamoja ambaye pia anayemsimamia, kutokea kutoelewana kiasi cha kususa kumsimamia kazi zake bila taarifa yoyote, licha ya kwamba ...

Mwanamuziki Rihanna hatakiwi kufika ghana

Image
Mwanamuziki wa kimataifa Rihanna anategemewa kuhudhuria mkutano mkubwa nchini Senegal,lakini vikundi vya dini nchini humo wamekataa kumpokea, chombo ch habari cha Jeune Afrique kimeripoti. "Tumeukataa ufreemason na mapenzi ya jinsia moja" , shirika la vikundi 30 vya kidini wamesema, wakimshutumu mwaimbaji huyo kwa kutumia ishara za mazo na kuwa mjumbe wa chimbuko la Illuminati , lilanoaminika kuwa ni kundi maalum la watu ambao hudhibit masuala na uongozi wa dunia na inasadikika kuwa hufanya shughuli zao kisiri kudhibiti kila kitu na kuunda Utawala Mpya wa Dunia. Shutuma hizo zimefutiliwa mbali na wasanii waliowahi kufanya nao kazi huko nyuma, Rihanna atatembelea nchi hiyo ya Afrika Magharibi akiwa katika nyadhifa yake ya balozi wa shirika la elimu 'Global Partnership Foundation' Shirika hilo linamaadhui wa kuchangisha fedha za kuwafundishia mamilioni ya watoto na vijana katika nchi zinazoendelea. Chombo cha habari cha Jeune Afrique kimemnukuu Waziri wa M...

Antonio Rudiger: Chelsea wamnunua beki kutoka Ujerumani

Image
  Antonio Rudiger alisaidia Ujerumani kushinda Kombe la Mabara mwaka 2017 nchini Urusi  Mabingwa wa Ligi Kuu ya England Chelsea wamemnunua beki Mjerumani Antonio Rudiger kutoka klabu ya AS Roma kwa mkataba wa miaka mitano kwa £29m. Rudiger, 24, alikamilisha uhamisho wake wiki moja baada ya kusaidia mabingwa wa dunia Ujerumani kushinda Kombe la Mabara. "Ni jambo linalonifurahisha sana kwa sababu si kila mchezaji anayepata fursa ya kujiunga na klabu kubwa kama hii," alisema Rudiger. Ada waliyolipa Chelsea inaweza ikapanda na kufikia £33.3m ukiongeza vikolezo vilivyo kwenye mkataba wake. "Antonio bado ana umri mdogo lakini ana uzoefu katika ngazi ya klabu na kimataifa na ana sifa zote ambazo zinahitajika kufana katika Ligi ya Premia," mkurugenzi wa kiufundi wa Chelsea Michael Emenalo alisema. "Ni mchezaji ambaye uwezo wake umethibitishwa." Rudiger atavalia jezi nambari mbili ambayo iliachwa wazi baada ya Branislav Ivanovic k...

Hadi kufikia August 2016, TOP 10 ya wanasoka wanaolipwa mkwanja mrefu

Image
Najua unajua kwamba mchezo wa soka ndio mchezo maarufu zaidi, kama ambavyo ulivyo maarufu na kupendwa na watu wengi ni kawaida kuona wanasoka pia wakilipwa pesa nyingi katika vilabu vyao hata katika mikataba yao ya matangazo ya kibiashara. Leo September 6 2016 mtu wangu wa nguvu nimekutana na list ya TOP 10 ya mastaa wa soka wanaongoza kwa kulipwa mkwanja mrefu, list kutoka mtandao wa  www.alux.com hadi kufikia  August 2016  hii ndio ilikuwa list ya wanasoka wanaoongoza kwa kulipwa mkwanja mrefu. 10. JAMES RODRIGUEZ ($21 MILLION ZAIDI YA TSH BILIONI 45) James Rodriguez 9. CESC FABREGAS ($21 MILLION BILIONI ZAIDI YA TSH BILIONI 45) Cesc Fabregas 8. EDEN HAZARD ($22 MILLION ZAIDI YA TSH BILIONI 48) Eden Hazard 7. LUIS SUAREZ ($23 MILLION ZAIDI YA TSH BILIONI 50) Luis Suarez 6. SERGIO AGUERO ($24 MILLION ZAIDI YA TSH BILIONI 52) Sergio Aguero 5. WAYNE ROONEY ($26 MILLION ZAIDI YA TSH BILIONI 56) Wayne Rooney 4. GARETH...