Alexis Sanchez ahukumiwa kifungo cha miezi 16 jela
Mchezaji mpya wa klabu ya Manchester United Alexis Sanchez amehukumiwa jela miezi 16 kutokana na kosa la kukwepa kulipa kodi.
Hukumu hiyo imetolewa jana ,Sanchez anadaiwa kukwepa kulipa kodi wakati alipokuwa nchini Uhispania ambapo mamlaka nchini humo zinasema anadaiwa kiasi cha pauni laki tisa.
Kwa mujibu wa sheria za Hispania, hukumu ya kosa hilo haizidi miaka miwili jela, lakini badala yake kulipa pauni 525,000 kutokana na kosa ambalo alilifanya miaka mitatu alipokuwa akichezea klabu ya Barcelona.
Hukumu ya Sanchez imekuja katika kipindi ambacho bado mamlaka za mapato nchini Hispania zinafanya uchunguzi kuhusu kocha Jose Mourinho anaye tajwa
Comments
Post a Comment