Historia ya Kanisa Katoliki duniani
Kanisa Katoliki likiwa la zamani ( Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki wanashiriki sifa hiyo) na kubwa kuliko madhehebu yote ya Ukristo , historia yake inashika sehemu muhimu ya historia ya Kanisa lote duniani tangu lilipoanza mwaka 30 hivi BK hadi leo. Baada ya Yesu Kristo kuhubiri na kukusanya wafuasi kati ya Wayahudi wa karne ya 1 , hao walitumwa naye duniani kote, hasa wanaume 12 aliowaita Mitume , yaani "waliotumwa". Waandamizi wao katika uongozi wa Kanisa walianza kuitwa maaskofu , na kati yao yule wa Roma alizidi kushika nafasi ya pekee kwa sababu Mtume Petro alifia dini katika mji huo kutokana na dhuluma dhidi ya Ukristo ambayo ilianzishwa na Kaisari Nero ( mwaka 64 ) na kuendelea kwa kwikwi hadi ilipoko...