Makala hii ni sehemu ya Kitabu cha Kalamu kwa Vijana ambacho kipo katika hatua za mwisho kuchapishwa. Mwandishi ameamua kutoa sehemu hii ya makala isomwe na watu wote baada ya tukio la ajali ya kusikitisha iliyopoteza maisha ya watoto 29. Haki zote za mwandishi zimehifadhiwa . Utangulizi Kati ya mambo ambayo binadamu tunayaogopa sana mojawapo ni kifo, mwanadamu anaogopa kifo kwa kuwa kwanza kinamtenga na familia yake, ndugu, jamaa marafiki ambao amezoeana nao, pili anaogopa kifo kwa kuwa hafahamu ni wapi anapoelekea, jambo lingine linalowaogopesha watu juu ya kifo ni kuyaacha mambo ya dunia na raha zake ambazo amekua akizihangaikia kwa muda mrefu sana, kifo huogopwa pia kutokana na hukumu kwa wale wanaoamini uwepo wa Mungu na hukumu yake. Mwanadamu anapofariki huku nyuma huacha majonzi na simanzi kubwa haswa kwa wale waliokua wanamtegemea na wote ambao kwa namna moja au nyengine walikua wanafaidika na uwepo wake hapa duniani. Kifo cha kijana mara nyingi huwa ni pigo zaidi, m...