Posts

Showing posts from March 26, 2018

Maaskofu waonya kuhusu Umoja na amani ya Tanzania

Image
Baraza la maaskofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri chini Tanzania (KKKT) linasema umoja na amani ya Tanzania viko hatarini. Katika waraka wa ujumbe wa pasaka unaosambaa katika mitandao ya kijamii na kutarajiwa kusomwa kesho katika makanisa mbali mbali ya KKKT nchini Tanzania, baraza hilo limeorodhesha mambo kadhaa ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi hiyo. Waraka umeyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na utekaji, utesaji, kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa, mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi. "Kukosekana kwa mazingira ya haki na uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa katika chaguzi mbalimbali. Chaguzi zote zimeghubikwa na ubabe, vurugu, hila, na vitisho", imesomeka sehemu ya waraka huo Waraka umeongeza pia kwamba uhuru wa kujieleza, kutoa na kupokea habari umeendelea kutoweka nchini huku ukionya kubanwa na ha

Ujumbe wa Kwaresima 2018 kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania

Image
Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu ndiyo kauli mbiu inayoongoza ujumbe wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kwa mwaka 2018. Ni ujumbe unaozingatia matukio makuu matatu: Jubilei ya Miaka 150 ya Ukristo Tanzania Bara, Miaka 50 ya Tamko la Maaskofu kuhusu Mwelekeo na Hatima ya Tanzania na Maandalizi ya Uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwaka 2019. Wapendwa Familia ya Mungu, Na Watu Wote wenye Mapenzi Mema,  “Neema na iwe kwenu, na amani zitokazo kwa Mungu, Baba yetu” (Kol 1:2). Utangulizi Kama ilivyo ada ya Wakristo pote ulimwenguni, kwa kipindi cha siku arobaini kabla ya kuadhimisha Jumapili ya Ufufuko wa Bwana Wetu Yesu Kristo, Wakristo hutumia muda huo kufunga, kufanya toba na kufanya matendo ya huruma kwa wote wenye mahitaji huku wakijitafakari kuhusu uhalisia wa hali yao ya kuwa ni wenye dhambi mbele ya Mungu, ili waweze kufanya toba ya kweli na yenye mageuzi na wongofu katika maisha. Mwaka huu kipindi hiki, kijulikanacho kama