“Mimi ni msichana nataka kubembelezwa” - Chemical

Msanii wa kike wa hip hop bongo Chemical, kwa mara ya kwanza amezungumzia maisha yake ya kimapenzi, kitu ambacho ni nadra sana kwa msanii huyo kufanya hivyo.
 

Akizungumza na team ya Planet Bongo ya East Africa Radio,  Chemical amesema yeye kama msichana ana hisia za mapenzi na anajua kupenda, ila anahofia kuumizwa hivyo hawezi nguvu nyingi kwenye masuala ya mapenzi.
“Unajua kuna mambo mengine tunayafanya kwenye muziki kuweza kuweka image nyingine, ila mi niko tofauti na niko real, ukisikiliza nyimbo zangu nyingi Chemical anajua kupenda, anataka kubembelezwa, mi msichana jamani, na mapenzi yapo, ila mimi nahisi nina vitu vini vya kufocus kiasi kwamba kwenye mapenzi sitii nguvu nyingi, sipendi moyo wangu uumie”, amesema Chemicla.
Chemical amefunguka hayo baada ya tetesi kuwa mpenzi wake alikuwa akiishi naye pamoja ambaye pia anayemsimamia, kutokea kutoelewana kiasi cha kususa kumsimamia kazi zake bila taarifa yoyote, licha ya kwamba alisaini naye mkataba.

Comments

Popular posts from this blog

DOWNLOAD NA USIKILIZE NYIMBO ZA KWARESIMA