Mfahamu Mfalme Mswati na wake zake
Mpaka sasa ana jumla ya wake 14 na watoto 24, wake zake wawili huchaguliwa na wazee wa nchi ambao hujulikana kama bodi, na lazima wawe wametoka kwenye familia zenye status nzuri.
Mke wake wa kwanza 'Queen LaMatsebula' ndiye anayehusika na masuala yote ya kiserikali, na lazima atokee kwenye familia yenye uwezo au wa kichifu, na awe na tabia na siha njema. Lakini licha ya kuwa ndiye mke mkubwa, mtoto wake wa kiume haruhusiwi kurithi kiti cha baba yake. Kitaaluma huyu ni mwanasaikolojia.
Mke wake wa pili Queen LaMotsa “La Madone” ambaye ni Patron wa shule ya wasichana ya Mt. Annes ya Malkerns na pia ni balozi wa UNDP, huyu huchaguliwa na bodi ya taifa (unaweza sema baraza la wazee) kuwa mke wa Mfalme.
Mke wake wa 3, Inkhosikati LaMbikiza ambaye ni mwanamuziki wa nyimbo za Injili, huyu ndiye mwanamke wa kwanza kuchaguliwa na yeye mwenyewe mfalme kutokana na utamaduni wao. Pia ndiye malkia wa kwanza wa Swaziland kurekodi albam ya muziki na kuendelea na msomo akiwa kama mke wa mfalme, ana degree ya sheria kwa upande wa taaluma. Na ndiye mama wa binti mkubwa wa Mfalme Mswati , Princess Sikhanyiso Dlamini, ambaye ni mwanamuziki wa kuimba na Hip Hop.
Mke wa 4, Inkhosikati LaNgangaza, huyu huchaguliwa na mwenyewe Mfalme Mswati, ambaye kitaaluma ni Wakili, anapenda masuala ya urembo na amekuwa akihamasisha sana masuala ya urembo kwa wanwake, elimu, afya ya uzazi na ni Matron wa Swaziland Hospice at Home , ambayo ilikuwa ikiendeshwa na Princess Diana mwenyewe wa Uingereza.
Mke wa 5, Inkhosikati LaHwala huyu alichaguliwa na mwenyewe Mfalme, na inasemekana alikimbia nchi na kwenda kuishi Afrika Kusini, sababu ya kufanya hivyo haijaelezwa lakini kisheria bado ni mke wa mfalme. Alipoondoka aliacha watoto watatu.
Itaendelea.............
Mke wake wa kwanza wa Mfalme Mswati, Queen LaMatsebula
Mke wake wa pili Queen LaMotsa “La Madone”
Mke wake wa 3, Inkhosikati LaMbikiza ambaye ni mwanamuziki wa nyimbo za Injili
Mke wa 4, Inkhosikati LaNgangaza.
Mke wa 5, Inkhosikati LaHwala, wa pili kutoka kulia.
Princess Sikhanyiso Dlamini, mtoto wa kwanza wa kike wa Mfalme Mswati ambaye ni mwanamuziki, anaimba na kurap
Comments
Post a Comment