"Nisijekufa nipo CCM nikaishia motoni"-Tambwe Hiza

Mhe. Freeman Mbowe amefunguka na kusema kuwa amesikitishwa na taarifa ya kifo cha Tambwe Richard Hizza na kudai kuwa alipotoka CCM na kwenda upinzani kwake yeye ni kama alikuwa anatubu kwani hakutaka kufa akiwa ndani ya CCM.

 Mbowe amesema hayo leo Februari 8, 2018 baada ya kusikia taarifa ya kifo cha Tambwe Richard Hizza ambaye amefariki ghafla usiku wa kuamkia leo 
"Nimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Kamanda Tambwe Richard Hizza, Kamanda mwingine tena amelala.Kamanda vita vizuri umepigana, safari umemaliza, hakika umesimama imara kuipigania demokrasia, hakika Taifa litakukumbuka kwa uthubutu wako wa kuikemea Serikali katika mabaya bila woga ingawa tulikuwa kwenye kipindi ambacho kumekuwa na kuminywa kwa haki ya kutoa mawazo na kuikosoa Serikali bila hofu" 
Kufuatia kifo cha Hizza Mwenyekiti wa CHADEMA amedai wao ili kumuenzi kamwe hawawezi kurudi nyuma bali watasimamia yale wanayoyaamini ili kumuenzi na kufikia matamanio ambayo kiongozi huyo alikuwa akiyatamani.
"Umekuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika timu ya Upinzani, tunakuahidi hatutarudi nyuma ili kukuenzi mpaka kufikia matamanio uliyoyatamani kuyaona katika Taifa letu, tunaamini safari ya kuelekea mabadiliko ya kweli bado kilomita kidogo tufike. Wewe ni shujaa, Nakuombea kwa Mungu akupokee na upumzike kwa amani, ulisema " Nimerudi Upinzani kutubu baada ya kuona umri na siku zimekwenda, nisijekufa nipo CCM nikaishia motoni" alisema Tambwe Hizza tarehe 07/02/2018 Tandale katika kampeni za kumnadi mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni kupitia CHADEMA, Salum Mwalim.
Tambwe Richard Hizza amekuwa akishiriki katika kampeni za mgombea Ubunge wa jimbo la Kinondoni toka siku ya ufunguzi wa kampeni hizo Januari 27,2018 na siku moja kabla ya kifo chake alishiriki kampeni za kumnadi mgombea wa Ubunge kupitia CHADEMA.
Upumzike kwa amani Tambwe Hizza, Inna lillah wa inna ilayhi raji'un.

Comments

Popular posts from this blog

DOWNLOAD NA USIKILIZE NYIMBO ZA KWARESIMA