Mtulia amkana Salum Mwalimu hadharani
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia amemkana mgombea
ubunge wa CHADEMA, Salum Mwalimu kwamba hakuwahi kumpigania kwa namna
yoyote wakati wa uchaguzi mkuu 2015 alipokuwa mgombea wa jimbo hilo
kupitia CUF chini ya mwamvuli wa UKAWA.
Mtulia amesema kwamba, Mwalimu kumuambia kwamba alimpigania si kweli kwani wakati wakati wa uchaguzi 2015, Mwalimu alikuwa anampigania mgombea mwingine wa jimbo la kikwajuni hivyo ana uhakika kwamba Mwalimu, (ambaye wakati huo alikuwa Katibu Mkuu) hakumpigania na kama yeye ndiye aliyempigania basi angejipigania mwenyewe ili ashinde.
Aidha Mtulia ameongeza kwamba "Mimi nimejiuzulu kwa sababu ya maslahi ya wana kinondoni. Yale niliyokusudia kuyafanya kama tungekuwa na serikali ya UKAWA ambayo kiongozi wangu alikuwa akiipigania tungeyafanya, kwa kuikosa serikali ya UKAWA tukabaki ukiwa. Wananchi wangu waelewe kwamba Mbunge wao nimehamia huku kwa ajili ya maslahi yao kuliko kuendela kupokea mishahara na posho tu.
Mtulia mwaka 2015 alishinda uchaguzi wa jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CUF ambayo ilikuwa chini ya mwamvuli wa UKAWA unaounganisha vyama vinne vikiwepo, CHADEMA, CUF, NCCR na NLD.
Comments
Post a Comment