Tundu Lissu amjibu Lemutuz

Tundu Lissu ametumia ukurasa wake wa Instagram kumjibu Lemutuz na kudai kuwa hajawahi kuwasiliana naye kwa namna yoyote ile na kama kweli angekuwa ni rafiki yake toka aliposhambuliwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana basi angeweza kumkumbuka japo hata kwa kumpa pole lakini hakufanya hivyo.
"Leo nimeonyeshwa post iliyopo kwenye Instagram account ya William Malecela aka Lemutuz. Kwenye post yake, Lemutuz amedai kwamba mimi ni rafiki yake mkubwa na wa miaka mingi, kabla vijana wengi wanaopiga makelele mitandaoni hawajazaliwa. Lemutuz ameeleza kwamba mwaka 2010 alinipokea Uwanja wa Ndege wa John F. Kennedy, mjini New York, nilipoenda kwenye mahafali ya dada yangu. Naomba kuweka ukweli wa kauli za Lemutuz wazi ili kuweka rekodi sawa. Kwanza, nimemfahamu Lemutuz tangu mwezi Mei, 2011. Nilikutana naye mara ya kwanza kwenye mahafali ya mdogo wangu kaka (sio dada) Vincent Mughwai, aliyekuwa anasoma Bridgeport University (sio Connecticut State University). Kama nakumbuka vizuri, Lemutuz alikuwa MC kwenye shughuli hiyo. Na siku hiyo kulikuwa na Watanzania wengine wengi waishio Marekani. 
Tundu Lissu alizidi kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo kuwa 
"Lemutuz hakunipokea mimi JFK wala kunipeleka Bridgeport, Connecticut, kwenye gari yake binafsi. Hatukuwa tunafahamiana kabla ya kukutana kwenye graduation ya kaka Vince, siku kadhaa baada ya mimi, mke wangu na ndugu zangu wengine kuwasili Marekani. Pili, ni kweli tulipiga picha ambayo ameitoa kama uthibitisho wa 'urafiki' wetu. Siku hiyo, kama ilivyo kwenye shughuli kama hizo, nilipiga picha na Watanzania karibu wote waliohudhuria graduation hiyo. Kama Lemutuz, wengi wa niliyopiga nao picha nilikuwa siwafahamu kabisa kabla ya kukutana nao siku hiyo. 
"Tatu, tangu siku hiyo sijawahi kufanya mawasiliano na Lemutuz ya aina yoyote. Nakumbuka tu kukutana na kusalimiana nae bungeni mwaka 2012, wakati alipokuja Dodoma akitaka kugombea ubunge wa Afrika Mashariki. Mimi sijajua sababu ya Lemutuz kutaka kulazimisha urafiki na mimi usiokuwepo. Yeye ni rafiki mkubwa wa Bashite na mpiga debe wa Rais. Tangu nimepigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na wanaoitwa 'watu wasiojulikana', rafiki yangu mkubwa huyu hajawahi kunitumia hata kadi ya pole. Huu ni urafiki feki wa kuwadanganyia Watanzania wasioelewa" alisisitiza Tundu Lissu 
Tundu Lissu kwa sasa yupo nchini Ubelgiji akifanyiwa matibabu zaidi kufuatia kushambuliwa na risasi na watu wasiojulikana mwaka jana akiwa mjini Dodoma Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya (CHADEMA) Mhe. Tundu Lissu amefunguka na kumtaka William Malecela aka Lemutuz kutotaka kulazimisha urafiki na yeye na kuwa yeye hawezi kuwa rafiki yake kama ambavyo anadai. 

Comments

Popular posts from this blog

DOWNLOAD NA USIKILIZE NYIMBO ZA KWARESIMA