Posts

listen & Download New Audio | Kcee ft. Sarkodie – Burn

Image

New AUDIO: Orezi ft. Tekno – Whine For Daddy

Image
Orezi collaborates with Tekno on his first single of 2018 titled ‘Whine for Daddy.’ The song comes after his 2017 hit songs, ‘Hallelujah’ and ‘ Cooking Pot ’. Orezi describes ‘Whine for Daddy’ as a “Sugar Daddy jam” aimed at making people dance. According to him, “I was just trying to make a record that people can dance to, just whine and Daddy will take care of you.”

“Mimi ni msichana nataka kubembelezwa” - Chemical

Image
Msanii wa kike wa hip hop bongo Chemical, kwa mara ya kwanza amezungumzia maisha yake ya kimapenzi, kitu ambacho ni nadra sana kwa msanii huyo kufanya hivyo.   Akizungumza na team ya Planet Bongo ya East Africa Radio,  Chemical amesema yeye kama msichana ana hisia za mapenzi na anajua kupenda, ila anahofia kuumizwa hivyo hawezi nguvu nyingi kwenye masuala ya mapenzi. “Unajua kuna mambo mengine tunayafanya kwenye muziki kuweza kuweka image nyingine, ila mi niko tofauti na niko real, ukisikiliza nyimbo zangu nyingi Chemical anajua kupenda, anataka kubembelezwa, mi msichana jamani, na mapenzi yapo, ila mimi nahisi nina vitu vini vya kufocus kiasi kwamba kwenye mapenzi sitii nguvu nyingi, sipendi moyo wangu uumie”, amesema Chemicla. Chemical amefunguka hayo baada ya tetesi kuwa mpenzi wake alikuwa akiishi naye pamoja ambaye pia anayemsimamia, kutokea kutoelewana kiasi cha kususa kumsimamia kazi zake bila taarifa yoyote, licha ya kwamba ...

"Nisijekufa nipo CCM nikaishia motoni"-Tambwe Hiza

Image
Mhe. Freeman Mbowe amefunguka na kusema kuwa amesikitishwa na taarifa ya kifo cha Tambwe Richard Hizza na kudai kuwa alipotoka CCM na kwenda upinzani kwake yeye ni kama alikuwa anatubu kwani hakutaka kufa akiwa ndani ya CCM.  Mbowe amesema hayo leo Februari 8, 2018 baada ya kusikia taarifa ya kifo cha Tambwe Richard Hizza ambaye amefariki ghafla usiku wa kuamkia leo  "Nimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Kamanda Tambwe Richard Hizza, Kamanda mwingine tena amelala.Kamanda vita vizuri umepigana, safari umemaliza, hakika umesimama imara kuipigania demokrasia, hakika Taifa litakukumbuka kwa uthubutu wako wa kuikemea Serikali katika mabaya bila woga ingawa tulikuwa kwenye kipindi ambacho kumekuwa na kuminywa kwa haki ya kutoa mawazo na kuikosoa Serikali bila hofu"  Kufuatia kifo cha Hizza Mwenyekiti wa CHADEMA amedai wao ili kumuenzi kamwe hawawezi kurudi nyuma bali watasimamia yale wanayoyaamini ili kumuenzi na kufikia matamanio ambayo kiongozi h...

Mtulia amkana Salum Mwalimu hadharani

Image
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia amemkana mgombea ubunge wa CHADEMA, Salum Mwalimu kwamba hakuwahi kumpigania kwa namna yoyote wakati wa uchaguzi mkuu 2015 alipokuwa mgombea wa jimbo hilo kupitia CUF chini ya mwamvuli wa UKAWA.   Leo asubuhi kupitia kipindi cha East Africa Breakfast ndani ya EA radio Mtulia ambaye ni mgombea wa Ubunge wa Knondoni kupitia CCM  ameyasema hayo wakati akijibu swali la Salum Mwalimu ambaye ni mshindani wake kwa sasa katika uchaguzi huo kupitia CHADEMA, baada ya kumuuliza anajisikia vipi baada ya kuwasaliti wana kinondoni ambao,  baadhi yao walipoteza maisha yao  wengine kubaki vilema na hata wajawazito kupoteza mimba zao wakati wakishinikiza mgombea wao (Mtulia) atangaziwe ushindi 2015. Mtulia amesema kwamba, Mwalimu kumuambia kwamba alimpigania si kweli  kwani wakati wakati wa uchaguzi 2015, Mwalimu alikuwa anampigania mgombea mwingine wa jimbo la kikwajuni hivyo ana uhakika kwamb...

Tundu Lissu amjibu Lemutuz

Image
Tundu Lissu ametumia ukurasa wake wa Instagram kumjibu Lemutuz na kudai kuwa hajawahi kuwasiliana naye kwa namna yoyote ile na kama kweli angekuwa ni rafiki yake toka aliposhambuliwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana basi angeweza kumkumbuka japo hata kwa kumpa pole lakini hakufanya hivyo. "Leo nimeonyeshwa post iliyopo kwenye Instagram account ya William Malecela aka Lemutuz. Kwenye post yake, Lemutuz amedai kwamba mimi ni rafiki yake mkubwa na wa miaka mingi, kabla vijana wengi wanaopiga makelele mitandaoni hawajazaliwa. Lemutuz ameeleza kwamba mwaka 2010 alinipokea Uwanja wa Ndege wa John F. Kennedy, mjini New York, nilipoenda kwenye mahafali ya dada yangu. Naomba kuweka ukweli wa kauli za Lemutuz wazi ili kuweka rekodi sawa. Kwanza, nimemfahamu Lemutuz tangu mwezi Mei, 2011. Nilikutana naye mara ya kwanza kwenye mahafali ya mdogo wangu kaka (sio dada) Vincent Mughwai, aliyekuwa anasoma Bridgeport University (sio Connecticut State University). Kama nakum...

Mange Kimambi ahesabiwa siku na Sheikh

Image
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Al Haji Mussa Salimu amemjibu mwanadada mkosoaji wa mtandaoni Mange Kimambi kwa kudai kuwa huu ndiyo mwaka wake wa mwisho kutumia mikono pamoja na ulimi wake kutukana watu. Sheikh huyo amesema kwamba kutokana na kitendo hicho cha Mwanadada huyo kumuanika mtandaoni na kumtolea maneno machafu yeye kama kiongozi wa dini atarudi kwenda kushtaki katika mahakama ya mbinguni ambayo haina rushwa. Kauli hiyo ya Sheikh Mkuu imekuja ikiwa ni siku moja tangu ianze kusambaa picha yake mitandaoni na kuanza kutuhumiwa kuwa anashiriki katika kampeni za uchaguzi mdogo kukisaidia Chama Cha Mapinduzi " Tutarejea katika mahakama ya mbinguni kwani mahakama ya Mwenyezi Mungu haina rushwa na tutamuuliza  Mwenyezi Mungu kama alimpa Huyu Mange Kimambi ulimpa mikono kwa ajilli ya kudhalilisha na kuvunja heshma za watu. Amekuwa akiwatukana viongozi wa serikali lakini kwa hekima zao wamemnyamazia kimya"  Al Haji Mussa Salimu . Ameongeza kwamba " Tun...