Diego Costa apewa muda zaidi kupumzika Chelsea
Costa alifungia Chelsea mechi yao ya mwisho, fainali Kombe la FA walipolazwa na Arsenal Mshambuliaji Diego Costa amepewa muda zaidi wa kumpumzika na Chelsea, hatua iliyozidisha uwezekano kwamba huenda akaihama klabu hiyo majira haya ya joto. Mhispania huyo wa miaka 28 amehusishwa na kuhaam klabu hiyo baada ya kufahamishwa na meneja Antonio Conte kwamba hayupo kwenye mipango yake. Costa hakujiunga na wenzake kwa mazoezi Jumatatu. "Iliafikiwa kati yake na klabu kwamba anafaa kuchukua siku zaidi kupumzika," taarifa kwenye klabu hiyo ilisema. Costa anatarajiwa kutohudhuria mazoezi wiki hii. Mshambuliaji huyo alikuwa mchezaji pekee ambaye hakufika uwanja wa mazoezi wa Chelsea Cobham kando na Antonio Rudiger, ambaye alijiunga na klabu hiyo Jumapili. Costa aliwajulisha wanahabari kwamba Conte alikuwa amemwandikia ujumbe wa simu kwamba hakuwa kwenye mipango yake mwezi jana, na inaarifiwa kwamba msimamo wake haujabadilika....