Wayne Rooney: Ninasubiri kwa hamu sana kwenda Tanzania
Nyota wa soka wa
England Wayne Rooney, ambaye amekamilisha uhamisho wake kutoka
Manchester United na kurejea Everton amesema anasubiri kwa hamu sana
kuzuru Tanzania.
"Naisubiri sana kwa hamu na ghamu (safari ya kwenda Tanzania) - inafaa kuwa safari nzuri," aliambia runinga ya evertontv."Itakuwa nzuri sana na natumai kwamba nitaweza kuingia uwanjani na kucheza.
"Huwa vizuri sana unaposafiri na timu. Ni vizuri kuwa hotelini na wachezaji, kujumuika nao na kuwafahamu zaidi.
"Sijawahi kwenda Tanzania, na kwa hivyo nasubiri sana kwenda huko."
Rooney atakuwa kwenye kikosi cha Everton kitakachocheza mechi ya kujiandaa kwa msimu ujao katika taifa hilo la Afrika Mashariki.
Amesema ziara hiyo itampa fursa mwafaka ya kufahamiana na wachezaji wenzake wapya.
says Everton's pre-season trip to Tanzania provides the perfect opportunity for him to get to know his new teammates.
Rooney, anayeongoza kwa ufungaji mabao England alitia saini mkataba wa miaka miwili Goodison Park Jumapili.
Rooney alifika kwa mazoezi USM Finch Farm leo Jumatatu na anapangiwa kuungana na wenzake kwa safari hiyo ya Tanzania baadaye wiki hii.
Vijana hao wa Ronald Koeman watacheza dhidi ya mshindi wa Kombe la Super Cup la SportPesa, Gor Mahia kutoka Kenya, katika mechi ya kirafiki Alhamisi.
Mechi hiyo itakuwa ya kusherehekea udhamini mkubwa uliotolewa na Sportpesa kwa Everton.
Rooney, 31, tayari anafahamiana na baadhi ya wachezaji wa sasa wa Everton.
Amewahi kucheza pamoja na Morgan Schneiderlin, Michael Keane, Phil Jagielka, Leighton Baines na Ross Barkley baadhi ya klabu na wengine timu ya taifa.
Comments
Post a Comment