Harnaam Kaur ni mwanamke anayefuga ndevu
Harnaam Kaur ni mwanamke anayefuga ndevu
Nilikuwa na nywele zilizojaa usoni tangu nibalehe, ikafikia wakati ambapo nilifikiri iwapo nywele hizo zingeendelea kuota katika uso wangu nitazikubali na kuziruhusu kumea.
Nilichokozwa shuleni kutokana na nywele zilizokuwa zikimea usoni.
Wazazi wangu walikuwa na wasiwasi na hali yangu ya afya kwa jumla.
Uchunguzi wa hospitali ulibaini kwamba nina homoni nyingi za kiume ikilinganishwa na zile za kike swala linalosababisha kumea kwa ndevu hizo.
Nilijaribu kila njia kuzinyoa nywele zilizokuwa zikimea usoni mwangu.
Nilijaribu kubadili rangi ya ngozi, kunyoa, kutumia mafuta ya kuondoa nywele bila mafanikio.
Nilinyoa kila siku. Lakini nywele hizo ziliendelea kuwa nyeusi na ndefu zaidi.
Nilikuwa na marafiki walionitunza walionijali sana huku ndugu yangu akinisaidia sana.
Amekuwa mtu ambaye nimekuwa nikimtegemea sana.
Alikosana na marafikize walionichokoza nilipoanza kuwachilia ndevu zangu kumea.
Niliugua na kuchoka na uchokozi huo na nilitaka kupinga tamaduni za kijamii kuhusu urembo.
Kuna watu wengi ambao ni waathiriwa wa uchokozi na aibu za kimwili, kwa hivyo mimi huifanya kuwa kazi yangu kutoa hamasa na kuwasaidia watu kukabiliana na madhara ya tatizo hilo.
Nimegundua kwamba nina nguvu, mimi ni mrembo na mtu asiyeogopa.
Sikujua nina vipaji vyote hivi.
Wakati unapochokozwa kile unachosikia ni mambo mabaya kukuhusu.
Kwa hivyo wakati nilivyoanza kujipenda na msimamo wote huo dhidi yangu ndiposa nilianza kugundua kwamba mimi ni mrembo, nikijiambia kwamba nina thamani.
Niligundua kwamba mimi nina nguvu zaidi ya watu wanavyojua.
Wakati huohuo, sidhani nimefika kiwango ambapo najiamini sana.
Kutokana na hali yangu mwili wangu huwa unabadilika mara kwa mara kwa hivyo ninalazimika kuweka juhudi za kujikubali.
Kwa sasa nina ugonjwa unaobadili rangi yangu tumboni- ulianza kwa ghafla kwa hivyo nalazimika kuukubali.
Safari ya kujipenda ni swala linalofanyika katika kipindi cha miezi ama hata miaka.
Bado naendelea kubadilika, naendelea kukuwa na kila siku inayopita, najaribu kutafuta kitu kipya cha kujipenda.
Kuna watu wengi ambao wamesahau umuhimu wa kujipenda .
Tunataka watu wengine kutupenda, lakini iwapo hatuwezi kujipenda, ni vipi tutaweza kueneza mapenzi hayo na watu wengine?
Nimegundua kwamba stori yangu inawasaidia watu kukutana nami.
Wanaweza kujieleza kwangu ili niwasaidie."
Comments
Post a Comment