Mfalme Salman wa Saudi Arabia amefanya mabadiliko ya nyadhifa za jeshi na wizara mbalimbali, pamoja na kuteua naibu waziri wa kike akiwa na lengo la kuingiza kizazi kipya serikalini. Sababu za mabadiliko hazijulikani. Mfalme Salman wa Saudi Arabia ametangaza mabadiliko katika nafasi za juu za kijeshi na wizara mbalimbali nchini humo. Nyadhifa muhimu ya Mkuu wa Wafanyakazi wa Jeshi na za maafisa wengine wa kijeshi zimebadilishwa, wakati vita vikiwa vinaendelea nchini Yemen. Ufalme wa Saudia haukutoa sababu za kutokea mabadiliko hayo na wala haukutoa maelezo yoyote juu ya namna inavyopanga kuimarisha Wizara yake ya Ulinzi. Katika wakati ambapo Ufalme wake unakosolewa kimataifa kwa kuongoza mashambulizi ya anga nchini Yemen yanayoua raia wa kawaida kwa kulenga masoko, hospitali na maeneo mengine ya raia. Watu wapatao 10,000 wameuawa katika vita hivyo ambavyo Saudi Arabia anaiunga mkono serikali inayotambuliwa kimataifa dhidi ya waasi wa Houthi wanaoudhibiti mji mkuu wa Sana...