NEWS:.Washirika wa Rais wa zamani wa Burkina Faso wafikishwa mahakamani

Washirika wawili waandamizi wa Rais wa Burkina Faso aliyeondolewa madarakani, Blaise Compaore na takribani watu wengine 20 walifikishwa mahakamani jumanne wakituhumiwa kupanga jaribio la mapinduzi mwaka 2015 dhidi ya serikali ya mpito.
Waandamanaji waliokasirishwa na jaribio la bwana Compaore la kubadilisha katiba ili kuongeza utawala wake wa miaka 27 walifanikiwa kumuondoa madarakani na kumlazimisha kukimbia nchi jirani ya Ivory Coast hapo mwaka 2014.

Jenerali Gilbert Diendere
Jenerali Gilbert Diendere
Wanajeshi wa kikosi maalumu cha ulinzi wa rais wakiongozwa na Jenerali Gilbert Diendere, mshauri mkuu wa Compaore waliwachukua mateka maafisa wa serikali ya mpito mwezi mmoja kabla ya uchaguzi wa mwaka uliofuata.
Jaribio lao la kuchukua madaraka kwa wiki moja lilishindwa baada ya kuuliwa watu 14 na zaidi yaw engine 250 kujeruhiwa. Jenerali huyo anashtakiwa kwa kutishia usalama wa taifa, kufanya mauaji na shambulio.
Akiwa kizimbani alikataa kusema chochote huku akikaribiana na waziri wa zamani wa mambo ya nchi za nje anayetuhumiwa kupanga njama hiyo ya jaribio 

Comments

Popular posts from this blog

DOWNLOAD NA USIKILIZE NYIMBO ZA KWARESIMA