Posts

Saudi Arabia yafanya mabadiliko katika nyadhifa za jeshi na wizara

Image
Mfalme Salman wa Saudi Arabia amefanya mabadiliko ya nyadhifa za jeshi na wizara mbalimbali, pamoja na kuteua naibu waziri wa kike akiwa na lengo la kuingiza kizazi kipya serikalini. Sababu za mabadiliko hazijulikani. Mfalme Salman wa Saudi Arabia ametangaza mabadiliko katika nafasi za juu za kijeshi na wizara mbalimbali nchini humo. Nyadhifa muhimu ya Mkuu wa Wafanyakazi wa Jeshi na za maafisa wengine wa kijeshi zimebadilishwa, wakati vita vikiwa vinaendelea nchini Yemen. Ufalme wa Saudia haukutoa sababu za kutokea mabadiliko hayo na wala haukutoa maelezo yoyote juu ya namna inavyopanga kuimarisha Wizara yake ya Ulinzi. Katika wakati ambapo Ufalme wake unakosolewa kimataifa kwa kuongoza mashambulizi ya anga nchini Yemen yanayoua raia wa kawaida kwa kulenga masoko, hospitali na maeneo mengine ya raia. Watu wapatao 10,000 wameuawa katika vita hivyo ambavyo Saudi Arabia anaiunga mkono serikali inayotambuliwa kimataifa dhidi ya waasi wa Houthi wanaoudhibiti mji mkuu wa Sana...

NEWS:.Washirika wa Rais wa zamani wa Burkina Faso wafikishwa mahakamani

Image
Washirika wawili waandamizi wa Rais wa Burkina Faso aliyeondolewa madarakani, Blaise Compaore na takribani watu wengine 20 walifikishwa mahakamani jumanne wakituhumiwa kupanga jaribio la mapinduzi mwaka 2015 dhidi ya serikali ya mpito. Waandamanaji waliokasirishwa na jaribio la bwana Compaore la kubadilisha katiba ili kuongeza utawala wake wa miaka 27 walifanikiwa kumuondoa madarakani na kumlazimisha kukimbia nchi jirani ya Ivory Coast hapo mwaka 2014. Jenerali Gilbert Diendere Wanajeshi wa kikosi maalumu cha ulinzi wa rais wakiongozwa na Jenerali Gilbert Diendere, mshauri mkuu wa Compaore waliwachukua mateka maafisa wa serikali ya mpito mwezi mmoja kabla ya uchaguzi wa mwaka uliofuata. Jaribio lao la kuchukua madaraka kwa wiki moja lilishindwa baada ya kuuliwa watu 14 na zaidi yaw engine 250 kujeruhiwa. Jenerali huyo anashtakiwa kwa kutishia usalama wa taifa, kufanya mauaji na shambulio. Akiwa kizimbani alikataa kusema chochote huku akikaribiana na waziri wa zamani...

Mbowe, vigogo Chadema waachiwa baada ya kuhojiwa kwa saa tano

Image
Viongozi hao walitakiwa kuripoti polisi baada ya tukio la kupigwa risasi mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine wac hama hicho wameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa Kituo Kikuu cha Polisi tangu saa 6:50 mchana Viongozi hao walifika kituoni hapo leo Jumanne Februari 27, 2018 na kuachiwa saa 1:02 usiku, kuitikia wito wa polisi. Walikwenda kituoni hapo baada ya Mbowe kumaliza mkutano wake na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho yaliyopo mtaa wa Ufipa, Kinondoni. Mmoja wa mawakili wa viongozi hao, Frederick Kihwelo ameileza MCL Digital leo kuwa wote wameachiwa kwa dhamana kwa kutakiwa kuwa na mdhamini mmoja na kutakiwa kuripoti tena kituoni hapo Machi 5, 2018 saa 1 asubuhi. Amesema viongozi hao walianza kuhojiwa saa 8:30 mchana, baada ya kufanya mazungumzo ya tuhuma zinazowakabili. Februari 20, 2018 Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa viongozi sab...

NEWS..Saudi king replaces military chiefs in shake-up

Image
Add caption Image copyright GETTY IMAGES Image caption King Salman (C) acceded to the throne in 2015 Saudi Arabia has sacked its top military commanders, including the chief of staff, in a series of late-night royal decrees. Saudi King Salman also replaced the heads of the ground forces and air defences. The news was published by the official Saudi Press Agency (SPA), but no reason for the sackings was given. They come as the war in Yemen, where a Saudi-led coalition is fighting rebels, is nearing the end of its third year. Crown Prince Mohammed bin Salman, who is also the defence minister, is believed to be behind various recent shake-ups in the country. Last year dozens of prominent Saudi figures, including princes, ministers and billionaires, were locked up in Riyadh's five-star Ritz-Carlton hotel as  the prince led a drive against corruption and abuse of power . Image copyright REUTERS Image caption The Saudi-led coalition intervened in Yemen in March 2015 ...

South Africa: Ramaphosa stamps mark with cabinet reshuffle

Image
New South African President Cyril Ramaphosa has announced his cabinet, making substantial changes to ministerial positions. He reappointed Nhlanhla Nene as finance minister, reversing his sacking by the former President Jacob Zuma. Mr Zuma, who is facing charges of corruption, was forced to stand down earlier this month by his own party. Mr Ramaphosa took over, promising a "new dawn" for the country and pledging to be tough on corruption. "In making these changes, I have been conscious of the need to balance continuity and stability with the need for renewal, economic recovery and accelerated transformation," Ramaphosa said, while announcing the appointments in Pretoria on Monday night. He kept several ministers appointed by his predecessor, but other former allies of the former president were demoted or lost their jobs. Media caption Cheers and song as Ramaphosa elected South Africa president David Mabuzza, the deputy president of th...

Mabadiliko ya wapenzi yaliyogusa nyoyo za wengi Kenya

Image
Kwa wengi, mwezi wa Februari ambao kawaida umekuwa ukihusishwa na mapenzi unakaribia kufikia ukingoni, na wengi wameanza kuisahau Siku ya Wapendanao. Kwa Samuel Githae na Zipporah Njeri, siku hii maarufu kwa upendo ilikuwa mwanzo wa matukio ambayo yamechangia kuinuliwa kwao kutoka kwa maisha ya kutotambuliwa mjini hadi kuwa watu mashuhuri. Wamekuwa bila makao rasmi, wakilala barabarani, kwenye vituo vya filamu na wakati mwingine katika nyumba za marafiki zao. Lakini sasa watahamia katika nyumba mpya rasmi Jumamosi, ambayo wamelipiwa kodi na mhisani. Isitoshe, wataabiri ndege kwa mara ya kwanza kwenda likizoni katika hoteli moja ya ufukweni pwani ya Kenya wiki ijayo. "Siamini kwamba nitapanda ndege," Njeri aliambia BBC, akionekana mwenye furaha, akipigapiga mikono kama ndege anayejiandaa kupaa. Yote yalianza kutokana na wazo la mpiga picha Johnson Muchiri kutoka kwa kampuni ya Muchiri Frames, na wafanyakazi wenzake, kutaka kufanya jambo la kipekee. Jacinta N...

Kenya, Tanzania zapata 'muarubaini' wa kero zao

Image
Marais wa Kenya na Tanzania wameahidi kuboresha ushirikiano uliopo kati ya nchi zao na kuamrisha mawaziri wao kutafuta ufumbuzi juu ya masuala madogo madogo yanayojitokeza. Marais hao wamesema kuwa biashara iliyoko inafanyika bila vikwazo vyovyote na hivyo kuagiza tofauti zilizojitokeza katika baadhi ya bidhaa zimalizwe. "Kuna mambo madogo madogo yanajitokeza katika biashara kati ya Kenya na Tanzania, tunataka kwa haya yote Mawaziri wa Kenya na Mawaziri wa Tanzania mkae myatatue, sisi hatuna tatizo, mambo mengine madogo madogo mno, mambo ya viatu, nguo, ngano, gesi ni madogo sana, mnatakiwa myatatue nyinyi yasifike kwetu, sisi huku tuko sawa sawa" amesema Dkt Magufuli, tamko ambalo limeungwa mkono na Rais Kenyatta. Mazungumzo hayo yamejiri baada ya kukutana nchini Uganda ambapo Rais Uhuru Kenyatta na Rais John Magufuli wamewaagiza mawaziri wao kuyatafutia ufumbuzi masuala yenye kero ndogo ndogo ambazo hujitokeza kwenye maeneo ya biashara kati ya nchi hizo. M...