Posts
Historia ya Kanisa Katoliki duniani
- Get link
- X
- Other Apps
Kanisa Katoliki likiwa la zamani ( Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki wanashiriki sifa hiyo) na kubwa kuliko madhehebu yote ya Ukristo , historia yake inashika sehemu muhimu ya historia ya Kanisa lote duniani tangu lilipoanza mwaka 30 hivi BK hadi leo. Baada ya Yesu Kristo kuhubiri na kukusanya wafuasi kati ya Wayahudi wa karne ya 1 , hao walitumwa naye duniani kote, hasa wanaume 12 aliowaita Mitume , yaani "waliotumwa". Waandamizi wao katika uongozi wa Kanisa walianza kuitwa maaskofu , na kati yao yule wa Roma alizidi kushika nafasi ya pekee kwa sababu Mtume Petro alifia dini katika mji huo kutokana na dhuluma dhidi ya Ukristo ambayo ilianzishwa na Kaisari Nero ( mwaka 64 ) na kuendelea kwa kwikwi hadi ilipoko...
Ni nani ambae ni Mrithi wa Mtakatifu Petro?
- Get link
- X
- Other Apps
MNAMO 2002, Papa Yohana Paulo wa Pili alimwandikia barua askofu wa Limburg, huko Ujerumani, akifutilia mbali uamuzi uliofanywa na askofu huyo kuhusu suala la kutoa mimba. Papa alianza kutoa maagizo yake kwa kusema kwamba anawajibu wa kuhakikisha kuwa “makanisa yote yako katika hali njema na yana umoja kulingana na mapenzi ya Yesu Kristo.” Alidai kuwa ana mamlaka ya kufutilia mbali uamuzi uliofanywa na askofu huyo kwa sababu akiwa papa, yeye ndiye “mrithi wa Mtakatifu Petro.” Kulingana na tafsiri fulani ya Kanisa Katoliki, “Kristo alimweka rasmi Mt. Petro kuwa mkuu wa mitume wote.” Kanisa Katoliki linaendelea kudai kwamba “Kristo alisema kwamba Petro anapaswa kuwa na watu watakaomrithi katika cheo hicho; na kwamba maaskofu Waroma ndio warithi wake.”— New Catholic Encyclopedia (2003), Buku la 11, ukurasa wa 495-496. Hayo ni madai mazito. Je, wewe mwenyewe umewahi kuchunguza ukweli wa madai hayo? Ona majibu ya maswali haya matatu: (1) Je, Biblia inaunga mkon...