Shambulizi la al-Shabaab laua watu 18


Magari mawili yenye mabomu yameripuka katika mji mkuu wa Somalia Ijumaa na kuuwa watu 18 na wengine 20 kujeruhiwa, idara ya huduma za ambulance imesema.
Wakati huohuo kikundi cha al-Shabaab kimedai kuhusika na shambulizi hilo, shirika la habari la Reuters limeripoti.
Wakati wa mlipuko huo kulikuwa na mashambulizi ya bunduki karibu na ikulu ya rais, idara hiyo imesema.
“Mpaka sasa tumeipata miili 18 ya watu waliouwawa na wengine waliojeruhiwa kutoka katika eneo la shambulizi usiku huu,” Abdikadir Abdirahma, mkurugenzi wa huduma za ambulance za Amin ameiambia Reuters.
Wingu kubwa la moshi lilitanda karibu na ikulu na mapambano ya kutupiana risasi yalizuka karibu na jumba hilo, mtu aliyekaririwa na Reuters amesema ameshuhudia hilo.
Polisi na mashuhuda wa tukio hilo wamesema bomu la pili lililipuka kutoka katika gari ambalo lilikuwa limeegeshwa mbele ya hoteli mbali kidogo na ikulu ya rais.
Polisi wamesema bomu la kwanza lililipuka baada ya washukiwa wa kikundi cha al-Shabaab walipokaidi kusimama katika lango la kuingilia nyumba ya rais na walirusha risasi kwa walinzi wanao linda lango hilo.

Comments

Popular posts from this blog

DOWNLOAD NA USIKILIZE NYIMBO ZA KWARESIMA