Majaliwa awashauri CHADEMA kuhusu kuporwa ushindi

Waziri Mkuu wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amefunguka na kuwapa ushauri Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu tetesi za kuporwa ushindi wa Kata kadhaa ambazo wao wanaona walishinda na kuwataka kukata rufaa.


Kassim Majaliwa amesema hayo leo Februari 8, 2018 akiwa anajibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wabunge mbalimbali, ambapo Mbunge wa viti maalum CHADEMA Devotha Minja alitaka kufahamu kama ni sera ya Serikali ya awamu ya tano kupora ushindi kwa watu ambao wameshinda kihalali.
Devotha Minja alihoji suala hilo na kudai kuwa katika baadho ya Kata zikiwepo Kata ya Sofi Malinyi CHADEMA ilipata kura 1,908 wakati CCM ilipata kura 1,878, Kata ya Siuyi Singida CHADEMA ilipata kura 1,358 huku CCM ikipata kura 1,304 lakini katika Kata hizo CCM ilitangazwa kushindi dhidi ya CHADEMA, ndipo hapa Waziri Mkuu aliposema kuwa anaamini Tume ya Uchaguzi haiwezi kutangaza matokeo ndivyo sivyo.
"Sitarajii kama Tume ya Uchaguzi (NEC) inafanya kazi ya kutangaza walioshindwa na kuwaacha walioshinda na masuala haya ya tume serikali imeweka utaratibu na tumeunda chombo kinachoshughulikia chaguzi zote nchini Tume ya Uchaguzi (NEC) lakini chombo kingine ni ile kwenye Mamlaka ya Serikali za mitaa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa pamoja na vyombo hivyo lakini tunazo sheria zinazosimamia simamia uchaguzi na zote hizi zinasimamiwa na Tume" alisema Majaliwa
Majaliwa aliendelea kutoa ufafanuzi kuwa kwa mujibu wa Sheria hizo zinatoa nafasi kukutana na vyama mbalimbali ambavyo havijaridhika juu na matokeo ya uchaguzi hivyo alitumia nafasi hiyo kuwashauri CHADEMA kufanya hivyo ili kutafuta haki yao kama wanaona kuna haki imeporwa.
"Ipo Sheria inatoa miezi mitatu ya kukata rufaa juu ya hizo namba ulizosisoma mimi sina uhakika nazo, sasa Mhe Mbunge kama una uhakika na takwimu ulizosisoma kwamba hao wenye namba nyingi ndiyo walishinda lakini ametangazwa mwingine bado unayo fursa ya kukata rufaa kwa mujibu ya Sheria ya uchaguzi, kwa hiyo nikushauri kufuata chombo chetu na kwa kuwa sheria zipo na wewe una fursa ya kufuata sheria ile ili kupata haki yako ya msingi" 

Comments

Popular posts from this blog

DOWNLOAD NA USIKILIZE NYIMBO ZA KWARESIMA