Waziri Mwakyembe alivyokwenda kuwapokea Taifa Stars saa 9 usiku

Alfajiri ya July 9 2017 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilirejea Dar es Salaam Tanzania ikitokea Afrika Kusini ilipokuwa inashiriki michuano ya COSAFA 2017 na kupokelewa na waziri mwenye dhamana ya michezi Dr Harrison Mwakyembe, ambapo Tanzania katika michuano hiyo imemaliza kwa rekodi ya kumtoa mwenyeji katika robo fainali.


Taifa Stars imewasili Dar es Salaam ikiwa ni siku moja imepita toka iifunge Lesotho na kuibuka mshindi wa tatu katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu, Taifa Stars iliishinda Lesotho kwa mikwaju ya penati 4-2 na kufanikiwa kutwaa nafasi ya juu zaidi katika mashindano hayo kwa mara ya kwanza

Baada ya kurejea Dar es Salaam Taifa Stars inajiandaa na mchezo wake wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya CHAN July 15 katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, ambapo watacheza na majirani zao timu ya taifa ya Rwanda.

Comments

Popular posts from this blog

DOWNLOAD NA USIKILIZE NYIMBO ZA KWARESIMA