Chanjo ya ugonjwa wa gonorrhoea yapatikana
Wanasayansi nchini New Zealand wameonyesha kwa mara ya kwanza kwamba chanjo inaweza kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa gonorrhoea.
Watafiti
kutoka chuo kikuu cha Auckland wamegundua kuwa maambukizi ya ugonjwa
huo wa zinaa yameshuka kwa takriban theluthi moja miongoni mwa watu
ambao walipata chanjo dhidi ya homa ya manjano.Watafiti hao wamefuatilia kutoka kwa vijana milioni moja waliopata chanjo hiyo pindi kulipotokea ugonjwa wa homa ya manjano nchini New Zealand.
Gonorrhoea imekuwa taabu kutibika kwa sababu imezoea antibiotic.
Comments
Post a Comment