BREAKING: Waziri Ngeleja atangaza kurudisha Pesa za ESCROW ...
Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja leo July 10 ametangaza kurejesha pesa Tsh. milioni 40.4 za mgawo kutoka kwa Mfanyabiashara James Rugemarila ambaye inaelezwa alilipwa zaidi ya Bilioni 300 za ESCROW.
Akizungumza mbele ya Wanahabari William Ngeleja alizibainisha sababu kuu tano zilizomfanya afikie uamuzi huo wa kurejesha fedha hizo kutoka kwa James Rugemarila ambaye ni mmiliki wa VIP Engineering and Marketing Ltd.
1: Nilipokea msaada huu kama wapokeavyo Wabunge wengine, kwa nia njema, bila kujua kwamba James Rugemalira baadaye angekuja kuhusishwa na kashfa ya fedha za akaunti ya ESCROW kama ilivyo sasa.
2: Kwa vile sasa imedhihirika kwamba aliyenipa msaada huu anatuhumiwa kwenye kashfa ya akaunti ya ESCROW, nimepima na kutafakari, na hatimaye nimeamua, kwa hiyari yangu mwenyewe.
3: Nimeamua kurejesha fedha hizi hata kama aliyenipa msaada bado ni mtuhumiwa tu, kwa vile hajathibitika kupatikana na hatia, kwa sababu sitaki kuwa sehemu ya kashfa/tuhuma hizo.
4: Leo nina zaidi ya miaka 12 nikiwa kiongozi wa Umma, na pia niliwahi kuitumikia Wizara ya Nishati na Madini kwa takribani miaka mitano na nusu, lakini sijawahi kukumbwa na kashfa ya rushwa au ufisadi
5: Ninarudisha fedha hizi ili kulinda heshima na maslahi mapana ya nchi yangu, chama changu (CCM), Serikali yangu, Jimbo langu la Sengerema, familia yangu na heshima yangu mwenyewe.
Comments
Post a Comment