BREAKING: Kilichoamuliwa na Mahakama kuhusu kesi ya Halima Mdee
Halima Mdee ameachiwa kwa dhamana ya Milioni 10 na wadhamini wawili, ushahidi haujakamilika kesi imeahirishwa hadi August 7, 2017.
Katuga alidai kuwa July 3, 2017 katika
Ofisi za Chadema makao makuu, alimtukana Rais Magufuli kwa kumwambia ”
Anaongea ovyo ovyo, anatakiwa afunge break,”. Baada ya kusomewa kosa
hilo, Mdee alikana kosa.Wakili Katuga alisema upelelezi wa kesi hiyo
haujakamilika anaomba kesi iahirishwe.
Mdee amedhaminiwa kwa bondi ya shilingi milioni kumi na wadhamini wawili ambapo kesi imeahirishwa hadi Agosti 7, mwaka huu.
Comments
Post a Comment