Msafara wa Makamu wa Rais Samia Suluhu wapata ajali Mtwara


​Msafara wa makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan ambao ulikuwa unaelekea wilayani Tandahimba ukitokea ikulu ndogo ya rais Mtwara umepata ajali na kusababisha majeruhi  ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa Ligula kwa matibabu.
moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.
.

.Majeruhi wa Ajali hiyo wakipatiwa Huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa Hospitali ya Ligula. (Picha kwa hisani ya mtandao)

.
Ajali hiyo imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara
Majeruhi walioumia ni dereva  pamoja na wasaidizi wanne wa Makamu wa Rais.
Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa wa Makamu wa Rais kuacha njia na kupinduka, gari jingine lililokuwa limebeba waandishi wa habari wa channel ten, startv na clouds tv liliacha njia na nusura kupinduka.

Gari lililopata ajali likiwa limeharibika vibaya.

Barabara ya kutoka mtwara kuelekea Tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha hata kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka na kusababisha majeruhi.


Comments

Popular posts from this blog

DOWNLOAD NA USIKILIZE NYIMBO ZA KWARESIMA