MIX Majibu ya Zitto kuhusu kufanya mkutano wa chama licha ya zuio la polisi


August 25 2016 Jeshi la Polisi lilipiga marufuku mikutano yote ya kivyama ndani na nje ili kuzuia machafuko waliyodai yanaendelea kujitokeza katika kipindi hiki.
Jana September 5 2016 Chama cha ACT-Wazalendo kilikutana katika kikao chake cha kawaida kujadili mambo mbalimbali ya chama. Leo September 6 2016 chama hicho kimekutana na waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa tamko rasmi la kamati kuu ya chama cha ACT wazalendo iliyokaa jana kuhusu hali ya nchi.
Mbele ya waandishi wa habari Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe amejibu swali la kufanya mkutano wa ndani licha ya zuio la polisi……
>>>hatujapata taarifa yoyote ile ya kimaandishi ya kwamba mikutano ya kikatiba ya chama imezuiwa ndio maana jana tumefanya mkutano wa kamati kuu na hatukuona polisi kama walikuwepo labda askari kanzu sababu huo ni mkutano wa kikatiba kwa mujibu wa katiba ya chama’ 
Aidha Zitto Kabwe akitoa tamko rasmi la kamati kuu ya chama cha ACT wazalendo iliyokaa jana kuhusu hali ya nchi.
>>>’Ukuaji wa shughuli za kiuchumi kwa kipindi cha miezi sita ya kwanza ya serikali ya awamu ya tano umefanya kasi ya ukuaji kushuka kutoka 9%-5%Zitto
      by :millardayo

Comments

Popular posts from this blog

DOWNLOAD NA USIKILIZE NYIMBO ZA KWARESIMA