Posts

Ujumbe alioupokea Rais Magufuli kutoka kwa Rais Salva Kiir na Rais Nkurunziza

Image
Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit amemtumia ujumbe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akimuarifu kuwa hali ya usalama katika nchi hiyo imeanza kutengemaa. Rais Salva Kiir Mayardit amewasilisha ujumbe huo kupitia kwa Mjumbe wake Maalum Aggrey Tisa Sabuni ambaye pamoja na kuwasilisha ujumbe huo amesema Sudani Kusini imekamilisha nyaraka za azimio la kuridhia mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao umewasilishwa jana tarehe 05 Septemba, 2016 katika makao makuu ya Jumuiya Jijini Arusha. Aggrey Tisa Sabuni amesema Sudan Kusini ipo tayari kushirikiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika masuala mbalimbali yenye manufaa kwa wananchi ikiwemo biashara na uwekezaji na kwamba ni matumaini yake kuwa itapata ushirikiano mzuri. Kwa upande wake Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na taarifa za kutengemaa kwa hali ya amani nchini humo na kwamba ...

Awilo Longomba (Official Video) – Kwanga Pamba | Mp4 Download

Image
Awilo Longomba (Official Video) – Kwanga Pamba | Mp4 Download

AUDIO | MIRIAM PAUL - HAPO MWANZO | Mp3 Download

Image
AUDIO | MIRIAM PAUL - HAPO MWANZO | Mp3 Download

A.M ft Olamide (Official Video) – Ojaju | Mp4 Download

Image
A.M ft Olamide (Official Video) – Ojaju | Mp4 Download

AUDIO | IKUPA MWAMBeNJA - ADONAI | Mp3 Download

Image
AUDIO | IKUPA MWAMBeNJA - ADONAI | Mp3 Download

Audio | Baraka Da Prince – Inodae | Mp3 Download

Image
Audio | Baraka Da Prince – Inodae | Mp3 Download

Ilichokisema Serikali kuhusu taarifa za Makamu wa Rais kujiuzuru

Image
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan Ofisi ya Makamu wa Rais inakanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, ameomba kujiuzulu nafasi yake na kwamba taarifa hiyo ni ya uzushi na uongo haina ukweli wowote. Taarifa hiyo ni ya uchochezi inayolenga kuliweka Taifa kwenye taharuki.  Mhe. Makamu wa Rais yuko bega kwa bega na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili kuwaletea wananchi maendeleo. Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka wananchi na Watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa hiyo ambayo inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Viongozi wetu. Mwisho, Ofisi ya Makamu wa Rais inawasihi Watanzania kufanya kazi kwa bidii na wajiepushe na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu nchini.